Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia watuhumiwa watatu waliokuwa wakijiusisha na shughuli za utapeli maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma na Mikoa Jirani.
Akizungumza kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Marco G. Chilya jana Februari 23,2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi Mkoa Ruvuma alisema kuwa mnamo Tarehe 05.02.2026 matapeli hao walitapeli jumla ya 147,300,000 kwa wakala wa CRDB aitwaye Paulo Dainet Akwezo huko maeneo ya bombambili Manispaa ya Songea katika Nyumba ya Kulala wageni ya Mwendapole.
Kamanda Chilya – SACP alibainisha kuwa tarehe 5.02.2026 majira ya saa sita mchana huko maeneo ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Mwendapoli iliyopo Bombambili Songea Mjini Paulo Dainet Akweso ambaye ni wakala wa CRDB alifatwa na watu watatu ambao majina yako hayafahamu na kumlaghai kuwa wanataka kumpatia utajiri wa haraka hivyo walitaka awapatie kiasi cha fedha ili ziweze kufanyiwa dawa na kuzalishwa zaidi na kuwa tajiri mkubwa.
Baada ya wakala huyo kuambiwa hivyo alitoka katika nyumba hiyo ya kulala wageni ambayo alikuwa amepangisha na kwenda kwa mawakala wadogo wapatao tisa na kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi Milioni mia moja, Arobaini na saba na Laki tatu147,300,000) na kuwaambia kuwa anaenda kuwawekea fedha hizo katika akaunti zao za benk kama salio (Floats) ili waendelee kutoa huduma kwa wateja lakini wakala huyo hakwenda Benki kama alivyowaambia badala yake alienda nazo katika nyumba ya kulala wageni kama alivyoelekezwa na matapeli.
Wakala huyo baada ya kufika katika nyumba ya kulala wageni alikutana na matapeli hao na wakamwambia azitandaze pesa hizo kitandani kisha azipake mafuta na aondoke katika chumba hicho bila kukifunga ili malaika waweze kuzichukua pesa hizo na wataziludisha zikiwa zimeongezeka zaidi ya hapo awali. Wakala huyo alitekeleza maagizo kwa kuondoka na baada ya saa moja alirudi katika chumba hicho na kukuta pesa zote hazipo hivyo akaamini kuwa malaika wamezichukua na wakala huyo aliendelea kukaa chumbani humo kwa muda mrefu akisubili peza zirudi lakini hazikurudi ampaka muajili wa wakala huyo alipopata taarifa na kutoa taarfia kituo cha Polisi.
Baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa kutumia timu ya wabobezi wa upelelezi tulianza ufuatiliaji mkali juu ya tuklio hilo na ilipofika tarehe 17.02.2026 huko mtaa wa Uhindini Mkoa wa Dodoma tulifanikiwa kuwakakamata watuhumiwa wawili ambao ni Enosta Kelv Kangapi @ Boss hanuniwi, Miaka 36 na Kelvin Taravatory Kangapi, miaka 37 na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na tukio hilo wakishilikiana na mtuhumiwa mwingine Salva Kombas @ Chura ambaye naye tarehe 18.02.2026 alikamatwa maeneo ya Standi kuu Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
Hata hivyo baada ya upelelezi kiongozi wa Kundi hilo la utapeli aitwaye Enosta Kel Kangapi @ boss hanuniwi katika akaunti yake ilibainika kuwa na kiasi cha fedha cha Shilingi Milioni Themanini na nane (88,000,000) ambazo alikiri kuwa kiasi hicho n sehemu ya pesa walizotapeli kwa Wakala Paulo Dainet Akweso na fedha nyingin akiwa amenunua pikipiki nne na viwanja vitatu huko Mbinga.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamni kwa hatua zaidi za kisheria.