Latest Posts

WAWILI WAKAMATWA KWA MAUAJI YA FESTO CHAULA KILOSA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata Seletwi Samiji Mdamanya na Paulo Lukas Sumai wote wakiwa wafugaji na wakazi wa Kijiji cha Malangali Kata ya Tindiga Wilaya ya Kilosa, kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Festo Selias Chaula maarufu kwa jina la Walter, mkulima na mkazi wa Tindiga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Andrew Kantimbo inaeleza kuwa tukio hilo limetokea Septemba 23.2026 majira ya saa 7 mchana katika Mashamba ya Bondeni Kitongoji cha Legeza Mwendo Kijiji na Kata ya Tindiga Tarafa ya Masanze Wilaya ya Kilosa.

Kamanda Kantimbo amesema Festo Selias Chaula alijeruhiwa baada ya kukatwa kichwani kwa kitu chenye makali na kupigwa kwa vitu butu katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyomsababishia majeraha makubwa na hatimaye kufariki dunia katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.

Mara baada ya Jeshi la Polisi kupokea taarifa kuhusu tukio hilo, lilianza ufuatiliaji kwa kufika katika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa awali ambapo lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wawili.

Baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kilosa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Askari wakiwa wanatumia usafiri wa gari la Polisi Toyota Hilux na Pikipiki tatu za aina mbalimbali wakiwa njiani pamoja na watuhumiwa kundi la watu wanadaiwa ni Jamii ya wakulima waliokadiriwa kufika 200 walifunga barabara na kuanza kushambulia askari

Katika kukabiliana na vurugu hizo ili kuokoa maisha na mali, Askari walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao ambao wengi wao walikuwa na visu, mapanga, mishale, mikuki, marungu na mawe ambavyo wananchi hao walilazimika kukimbia.

Baada ya wananchi wale kukimbia Askari walifanya ukaguzi wa eneo la tukio ndipo walipobaini kuwa mtu mmoja kati ya wale waliokuwa wakiwashambulia Askari amejeruhiwa na kitu chenye makali maeneo mbalimbali ya mwili,Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Kelvin Mhagama, Mkulima Mkazi wa Kichangani, alifariki akiwa anapatiwa matibabu baada ya kufikishwa hospitali.

Aidha katika tukio hilo Askari Polisi watatu walishambuliwa silaha za jadi na kupata madhara mbalimbali katika miili yao na wote wanaendelea na matibabu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!