Latest Posts

WENYE MAHITAJI MAALUMU WAKUMBUKWA, ‘TUSIWAFICHE NDANI’.

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Jamii nchini hasa wazazi na walezi wametakiwa kuwatunza na kuwafichua watu wenye mahitaji maalumu ili wafurahie maisha na kuhakikisha wanapata haki sawa kama ilivyo kwa wananchi wengine badala ya kuwatenga.

Hayo yameelezwa na Dkt. Miriam Elisha kwenye hafla ya utoaji tuzo za ‘Malikia wa nguvu’ zilizoandaliwa na Clouds Media na kufanyika jijini Mbeya ambapo Dkt. Miriam ameibuka mshindi katika kipengele cha maboresho ya sekta ya elimu.

Akizungumza na kituo hiki baada ya kutangazwa mshindi, Miriam ameishukuru Serikali kwa kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu nchini ikiwemo kwa watu wenye mahitaji maalum huku akitaka viongozi kuanzia ngazi za vitongoji, vijiji na ngazi za juu kushirikiana na wananchi kuhakikisha watu wenye mahitaji mbalimbali wanahudumiwa kwa kupata mahitaji yao yote bila ubaguzi wowote ikiwemo kuwaficha ndani hivyo kukosa haki zao.

Hata hivyo mshindi huyo wa tuzo ya Malikia wa nguvu mwaka 2025 kwenye sekta ya elimu amewataka wananchi kutojidharau badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wake Lightness Ndelwa, amewataka wanawake kutokata tamaa katika kuendelea kufanya kazi zao, jamii na Taifa kwa ujumla huku akiwashukuru baadhi ya viongozi wanaowapa mitaji kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

Clouds Media nchini Tanzania inatoa tuzo hizo kwa wanawake mbalimbali ili kutambua mchango na jitihada zao katika maeneo mbalimbali na kuwatia moyo kuendelea kusonga mbele katika kufanya kazi na kusimama kwenye nafasi zao ili kufikia maendeleo endelevu

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!