Latest Posts

MTWARA WAOMBWA KUTUMIA FURSA YA UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

Uzalishaji mdogo wa maziwa nchini Tanzania umetajwa kuwa sababu kubwa ya kutofikia malengo ya kila mtanzania kunywa angalau lita 200 ya maziwa kwa mwaka.

Hayo yameelezwa Septemba 25,2024 na Prof. George Msalya Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania kwenye kilele cha siku ya Unywaji Maziwa shuleni
yenye kauli mbiu ya “Mpe mtoto maziwa, kwa maendeleo bora shuleni”Kilele cha maadhimisho hayo kimefanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.

Ameeleza kuwa Tanzania inazalisha maziwa lita bilioni 3.9 ambayo ni kidogo na hayatoshi kwa kila mtanzania kunywa lita 200 ambazo zimependekezwa na mashirika ya chakula duniani ya WHO na FAO.

Sambamba na hilo ametoa rai kwa wananchi mkoani Mtwara kutumia fursa ya ufugaji ng’ombe wa maziwa ili waweze kuongeza kipato kwani ngo’mbe mmoja wa maziwa anaweza kuwapatia faida kubwa ambapo kwa mwezi mmoja wanaweza kuingiza kati ya milioni 1 hadi milioni 2 ambayo ni zaidi ya mshahara wa watu wengine.

Lucy Mkope mwakilishi kutoka benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), ametoa wito kwa serikali na Chama Cha Mapinduzi CCM kuhamasisha ufugaji katika mkoa wa Mtwara kwani kuna uhitaji wa kuimarisha afya za watoto na jamii nzima kwa kupata maziwa.

“Niwaombe kutumia fursa za kupata uwezeshwaji wa kupata ng’ombe bora ambao wanaweza kutoa maziwa mengi ili kuendelea kuhamasisha unywaji wa maziwa na uzalishaji wa maziwa.”Amesema Mkope

Athumani Mpochi mwakilishi kutoka kampuni ya usambazaji wa maziwa ya Asasi amewataka wazazi kupata hamasa ya kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia watoto waweze kupata maziwa ili kujenga afya ya mtoto na kumuepusha na maradhi nyemelezi na kuchangia pato la taifa.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya ameiomba bodi ya maziwa kuona namna ya kuweka bei rafiki ya maziwa kwa ajili ya wanafunzi ili kila mwanafunzi aweze kumudu bei na kunywa maziwa kwa ajili ya kuupa mwili afya, akili na nguvu ikizingatiwa wanafunzi wengi huenda shuleni bila kupata chakula asubuhi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!