Latest Posts

MVTTC WAASWA KUTANGAZA KOZI YA UWALIMU WA UFUNDI STADI ILI KUONGEZA UDAHILI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore, ameutaka uongozi wa Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) kuongeza juhudi za kutangaza kozi zinazotolewa chuoni hapo ili kuvutia udahili wa wanafunzi zaidi.

Akizungumza tarehe 5 Desemba 2024, wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika chuo hicho, CPA Kasore alisema mahitaji ya walimu wa kufundisha vyuo vya ufundi stadi yanaongezeka kutokana na juhudi za serikali kujenga vyuo hivyo kila mkoa na wilaya nchini.

“Kwa sasa tuna vyuo vya VETA kila mkoa, na tunajenga vyuo katika kila wilaya. Vyuo hivi vyote vitahitaji walimu wa kufundisha, na chuo hiki cha MVTTC ndicho pekee kinachoandaa walimu wa ufundi stadi nchini,” alisema CPA Kasore.

Alisisitiza umuhimu wa MVTTC kutangaza kozi zake, ikiwa ni pamoja na programu zinazotolewa kwa masafa (outreach programs), ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wenye sifa na uhitaji wa mafunzo hayo.

Pia, Kasore alieleza mkakati wa VETA kupunguza utegemezi wa kifedha kutoka serikalini kwa kuongeza uzalishaji kupitia vyanzo vipya vya mapato. Alihimiza chuo hicho kutunza na kutumia vyema vifaa vya kufundishia vilivyopo kwa ajili ya mafunzo ya vitendo na uzalishaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha MVTTC, Samweli Kaali, aliahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu kwa lengo la kuboresha huduma za mafunzo chuoni hapo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!