Latest Posts

SABABU HIZI ZATAJWA KUCHOCHEA MATUKIO YA WATU KUJIUA/KUJINYONGA

Theophilida Felician , Kagera.

Maisha magumu, upweke, migogoro ya ndoa, wivu wa mapenzi,  madeni makubwa, msongo wa mawazo, ulevi uliopindukia na ramli chonganishi ni  miongoni mwa sababu zinazochangia kasi ya matukio ya watu kujitoa uhai kwa kujinyonga.

Kauli hiyo imetolewa na mchungaji wa kanisa la EAGT MLIMA WA AHADI Clavery Venant  wakati akizungumza na Blog hii  ofisini kwake manispaa ya Bukoba ambapo amesema  kutokana na jamii kukabiliwa na changamoto mbalimbali watu wamekuwa wakukata tamaa na matokeo yake kuchukua maamuzi yasiyo sahihi hususani ya kujiua matukio ambayo yameshika kasi kutokana na kuripotiwa mara kwa mara  maeneo mbalimbali nchini.

Amefafanua kuwa kujiua siyo maamzi sahihi ni maamzi mabaya kwani hali hii  imepelekea athari ya kuwapoteza watu  wanaoziacha familia  zikitangatanga kwa jamii hasa watoto yatima.

Mchungaji huyo amesema tatizo hilo limewakumba hata watoto wadogo kuchukua maamuzi hayo ya kujinyonga moja ya sababu ikiwa ni kutokupata malezi ya upendo wa dhati kwa wazazi kwani wazazi wamejisahau katika eneo hilo badala yake watoto wanajikuta wakilelewa na watu wengine wakiwemo ndugu wa familia na  wafanya kazi  wandani jambo ambalo limewapelekea baadhi yao kukutwa na ukatili dhidi ya vitendo vya ubakaji.

Ametoa wito kwa jamii kuachana na vitendo hivyo viovu wawashirikishe watu changamoto  zao ili kupata ushauri pamoja na kumcha Mungu yeye atawaponya  makovu ya maumivu yaliyoighubika  mioyo yao huku akiwasihi kutokutenda dhambi.

Hata hivyo amewashauri viongozi wa dini, wanasaikolojia na makundi mengine kujitokeza na kuwasaidia wananchi kuwapa elimu yenye ufahamu juu ya  madhara ya kujiua itaweza kuyapunguza na kuyadhibiti  matukio ya namna hiyo kwa jamii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!