Latest Posts

TAKUKURU IRINGA YAIWEZESHA TANROADS KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 106 ZA MAEGESHO

 

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Iringa imeisaidia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kukusanya shilingi 106,192,180 zitokanazo na matumizi ya hifadhi ya barabara katika maeneo ya maegesho ya magari.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kabla ya uingiliaji kati wa TAKUKURU, mapato hayo yalikuwa yakikusanywa isivyo rasmi na kuwanufaisha watu binafsi hali hiyo ilisababisha serikali kupoteza mapato, ambapo kwa mwaka mzima makusanyo yalifikia takribani shilingi milioni tisa pekee.

Hata hivyo, baada ya TAKUKURU kuanza ufuatiliaji na kuchukua hatua stahiki, ndani ya kipindi cha miezi mitatu tu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2025, jumla ya shilingi 106,192,180 zilikusanywa na kuwasilishwa serikalini kupitia TANROADS.

Maeneo yaliyohusishwa katika ufuatiliaji huo ni Ndiuka, Ifunda, Ilula Mtua na Ruaha Mbuyuni, ambako huduma za maegesho hutolewa katika hifadhi ya barabara.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mipango kutoka TANROADS Mkoa wa Iringa, Michael Anywandwile, ameipongeza TAKUKURU kwa hatua zake za kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali huku akisema mafanikio hayo yatawezesha wakala huo kuboresha huduma katika maeneo ya maegesho, ikiwemo ujenzi wa vyoo vya kisasa, uwekaji wa kamera za ulinzi na uimarishaji wa miundombinu mingine muhimu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!