Latest Posts

HECHE ASHANGAZWA KUJUMUISHWA JAJI WA UGANDA, NAMIBIA KWENYE TUME YA RAIS

Saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua Tume Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche ametoa msimamo mkali wa kuikataa tume hiyo, akiitaja kuwa ni mbinu ya kutaka kutengeneza picha isiyo halisi mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika wilaya ya Rorya mkoani Mara leo Agosti 07, 2026, Heche amesema kuwa CHADEMA haitambui tume hiyo na matokeo yake yoyote yatakayotolewa yatakuwa ni “feki”. Heche ametumia mfano wa ujenzi wa ghorofa juu ya tope kuelezea kutokuwa na imani na tume hiyo, akisema kuwa haiwezi kupata ukweli ikiwa inaongozwa na ripoti ya tume iliyopita.

Heche amekosoa vikali uamuzi wa kumjumuisha jaji kutoka Namibia, na Jaji kutoka nchini Uganda akidai kuwa nchi hiyo ina rekodi mbovu ya haki za binadamu na uhuru wa mahakama. Heche amesisitiza kuwa msimamo wa chama chake ni kuendelea kudai Katiba Mpya na msuluhishi wa kimataifa anayekubalika na pande zote.

Hata hivyo, Rais Samia ameelezea imani yake kuwa majaji wote waliopo kwenye Tume hiyo, watatumia uzoefu wao wa miaka mingi kutekeleza majukumu yao ndani ya miezi mitano ijayo kwa kwa “weledi, umakini, na uadilifu mkubwa”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!