Latest Posts

POLISI YAWASHIKILIA ASKARI WATATU WA NGORONGORO KUFUATIA KIFO CHA MAFUNDI MAGARI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia kwa uchunguzi askari watatu waliokuwa zamu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, kufuatia incident iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na mwingine kulazwa hospitalini baada ya kudaiwa kukamatwa ndani ya hifadhi hiyo.

Tukio hilo lilitokea baada ya watu hao watatu, ambao ni mafundi magari kutoka jijini Arusha, kudaiwa kukamatwa na askari wa hifadhi hiyo mnamo Agosti 12, 2026, wakituhumiwa kuingia katika eneo la hifadhi bila kufuata utaratibu na wakiwa na pikipiki.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, amebainisha kuwa jeshi hilo lilipokea taarifa ya watu wawili kufikishwa katika Hospitali ya Lutheran wilayani Karatu, ambapo mmoja wao alikuwa ameshatembea na mwingine akiendelea kupatiwa matibabu.

“Inadaiwa baada ya kukamatwa na kuhojiwa walieleza walikuwa wametokea jijini Arusha wakiwa na pikipiki kuelekea Babati kwenye msiba na wakapotea njia wakajikuta wapo kwenye hifadhi ya Ngorongoro,” amesema Kamanda Masejo.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa aliyefariki dunia ni Sefu Mussa, mwenye umri wa miaka 25 na mkazi wa Matejoo jijini Arusha, huku majeruhi anayeendelea na matibabu akitambulika kwa jina la Salimu Haji, maarufu kama Chambega. Mtu wa tatu aliyekuwa nao, Abdallah Nuru, alifanikiwa kurejea jijini Arusha.

“Aidha Askari watatu waliokuwa zamu katika eneo ambalo watu hao wanadaiwa kukamatwa wanaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi ili hatua nyingine za kisheria zifuate,” amesema Kamanda Masejo.

Akitahadharisha na kusimulia tukio hilo, Abdallah Nuru ameeleza kuwa walipotea njia wakati wakielekea msibani Babati na kujikuta wakipita katika gate la hifadhi hiyo, ambapo walipigwa na kupewa adhabu kali na askari hao wakituhumiwa kuwa ni majangili.

“Wakasema nyie mnadanganya ni majangili mlikuwa mnaenda kuwinda nini huko… tukawaambia hapa tumekosea njia. Wakasema tupaki pikipiki wakaanza kutupa adhabu wakatunyoosha miguu wenzangu wakawa wameshindwa wakaambiwa wavue nguo na kuwamwagiwa maji, wakaenda kuwalaza kwenye hiyo miiba kumbe bora uchomwe na kisu hiyo miiba inauma sana,” alidai Abdallah.

Abdallah ameongeza kuwa hali ya wenzake ilizidi kuwa mbaya kutokana na adhabu hizo na kupelekea mmoja wao kupoteza maisha wakiwa njiani kuelekea hospitalini kwa msaada wa msamaria mwema aliyewasaidia usafiri wa bajaji.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!