Latest Posts

SINA KESI YA KUJIBU SABABU NI HIZI/ LISSU ASISITIZA FIDIA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameieleza Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo Dar es Salaam kuwa hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili huku akiiomba mahakama kutamka kuwa hana hatia na itamke kuwa anatakiwa kulipwa fidia.

Akiwasilisha hoja zake leo Agosti 17, 2026  mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru Lissu akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(CPA) amesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha ile aliyoiita Prima facie case (kutokuwa na kesi ya kujibu).

Lissu ameieleza Mahakama kuwa kuwa Prima facie evidence/case ni ushahidi wa upande wa mashtaka pekee yake kama haujafikia kiwango cha kumtia mtuhumiwa hatiani usipojibiwa hakuna hatia na Mahakama inatakiwa kurekodi mtuhumiwa kutokua na hatia.

Akitumia kifungu cha 312(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na maamuzi ya Mahakama katika kesi kadhaa ikiwemo ya kesi ya Rambaklal Trambaklal Bhatt dhidi ya Jamhuri amesema zimetengeneza misingi ya kisheria  juu ya kitu gani mahakama inatakiwa kufanya kuhusiana na hoja ya kutokuwa na kesi ya kujibu.

Sababu ziliaoainishwa na mahakama hizo ni kuwa ni utiifu wa Jamhuri ya Muungano, lazima kuwe na uthibitisho wa nia ya kufanya kitendo cha uhaini na hiyo nia lazima ithibitishwe kwa maandishi au matendo ya wazi.

Anaeleza kuwa suala la utiifu kwa Jamhuri ya Muungano halina mjadala na suala lenye shida ni je kulikuwa na nia ya dhati ya kufanya uhaini akieleza kuwa katika maneno yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ambayo aliyatoa April 3, 2025 na pia kupitia ushahidi wa mashahidi 17 wa jamhuri hakuna sehemu alipoonyesha nia ya kuitisha serikali kwani hakuna sehemu ilipotamkwa.

Lissu anasema kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani ya mwaka 2023, Sheria ya Kanuni ya Adhabu na sheria zingine hazithibitishi kosa la uhaini analodaiwa kulifanya.

“Kuwa ule ushahidi unaotajiwa wa kuthibitisha uhaini kwamba lazima kuwa na uthibitisho wa nia ya kufanya kitendo cha uhaini haupo kuwa hakuna ushahidi wa nia ya kutenda josa lolote linalojulikana kwa sheria za tanzania kuwa jamhuri imeshindwa kuthibitisha Prima facie case na Kuwa kitu alichoshtakiwa nacho sio kosa kwa mujibu wa sheria zozote”

Ameeleza kuwa uchaguzi mkuu unaendeshwa na Tume ya uchaguzi na wala si serikali hivyo anasema kwa kuangalia hati ya mashtaka serikali haijatishiwa haijatajwa haisimamii uchaguzi akiuliza ameitamka wapi huku akiwataka Majaji kukumbuka kuwa yeye ndiye mshtakiwa pekee kwenye hiyo kesi  na shtaka lake linahusu maneno huku akirejea maamuzi ya Mahakama ya Rufani ambayo ilisema maneno ya mtu mmoja hayatengenezi kosa la uhaini.

Hoja nyingine ya Lissu ili kuwa mhaini lazima kuwe na uthibitisho wa kuandika/machapisho au matendo ya wazi ambapo anaeleza mbele ya Mahakama kuwa upande wa mashtaka kwenye shtaka lao na maelezo waliyoyaleta wakati wa kusikilizwa awali walidai kwamba Lissu amechapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV akiikataa tuhuma hiyo kuwa mchapishaji sio yeye bali ni shahidi wa kumi na saba(PW17)

Anaeleza kuwa mashahidi 17 wa Jamhuri walidai wameona video lakini haipo mahakamani akisema kama hakuna video hakuna kesi, hakuna uthibitisho kwamba alichapisha chochote mahali popote.

Hata hivyo aliwaomba Majaji kutazama ukurasa wa 135 kwa rekodi za Mahakama ambapo upande wa mashtaka uliorodhesha ushahidi wa nyaraka tisa video clip iliyopo kwenye flash video clip iliyopo kwenye memory card ripoti ya uchunguzi wa hizo video. Ushahidi wa aina tisa wa nyraaka mbili wa vielelezo visivyokuwa karatasi kuwa vipande vya ushahidi 11 vingeletwa lakini hakijaletwa hata kimoja.

Anasema uthibitisho wa kuchapisha/machapisho haupo wala uthibitisho wa matendo haupo kuwa kwenye kigezo hicho cha tatu na kama haijathibitishwa hakuna Prima facie case ya kuwafanya majaji wamuamuru ajitetee.

Aliendelea kuieleza Mahakama kwa nini hana kesi ya kujibu akisema kama hakuna uthibitisho wa nia wala uthibitisho wa machapisho maana yake hakuna Prima facie case akisema kuwa akiamriwa ajitetee majaji watakuwa wanakosea kisheria na wasipokubali wanafanya kile ambacho kifungu cha 312(1) cha CPA kinasema wafanye.

Aliewaleza jopo la Majaji watatu kuwa rai yake ni kutamoa kutokuwa na hatia na kama wakiridhika kuwa hana kesi ya kujibu aliomba watoe uamuzi huo leo na hukumu iandikwe halafu waitwe baadae kuja kusikiliza akieleza kuwa haipo sababu ya yeye kurudishwa ukonga kwani siku 495 ni nyingi sana

Anaeleza kwa ushahidi ulioletwa na upande wa mashtaka na mashahidi 17 kuwa ameshtakiwa kwa kosa lisilokuwepo kwenye vitabu vya sheria na amekaa gerezani siku 496 kwa kitendo ambacho sio kosa la uhaini na si kosa dhidi ya sheria zozote za nchini kwa mashtaka ambayo ni ya uonevu. Huku akiwaeleza majaji kuwa wana uwezo wa kuyafidia na kuhoji kwa msisitizo “Haya maumivu ya siku 495 atayalipia nani, nani atakayelipia maumivu ya familia yangu ya kutokuwa na baba yao kwa siku zote hizi.”

Pia aliomba kupangiwa tarehe ya kuthibitisha atafidiwaje ili ikitolewa amri kuwe na msingi wa ushahidi kwa sababu sina kesi ya kujibu sheria inataka muandike kutokuwa na hatia

Baada ya Lissu kumaliza hoja zake upande wa Jamhuri unaendelea na kesi kuieleza Mahakama ni kwa nini Lissu ana kesi ya kujibu.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!