Latest Posts

PPRA YANG’ARA KILELE MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2026

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imepongezwa kwa kuwezesha makundi maalum ya Watanzania kushiriki katika fursa za ununuzi wa umma, baada ya makundi 33,524 ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu kusajiliwa na kunufaika na mikataba 3,466 yenye thamani ya Sh bilioni 74.32 katika kipindi cha kuanzia Julai 1, 2023 hadi Oktoba 13, 2026.
‎
‎Takwimu hizo ziliwasilishwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang’onda, katika ripoti yake wakati wa kilele cha mbio hizo kilichofanyika Oktoba 14, 2026 katika Uwanja wa CCM Nelson Mandela mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa
‎
‎Katika hotuba ya kufunga mbio hizo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, aliipongeza PPRA kwa kuimarisha mifumo inayowawezesha wananchi kupata fursa za zabuni za Serikali.
‎
‎Kuona kwamba zaidi ya makundi 33,500 ya wananchi yamesajiliwa na kupata fursa za mikataba ya zabuni zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 74.32 ni ushahidi thabiti kuwa Serikali inafanya kazi kwa ajili ya Watanzania wote,” alisema Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi.
‎
‎Takwimu zilizowasilishwa katika ripoti hiyo zinaonesha kuwa vijana wanaongoza kwa idadi ya makundi yaliyosajiliwa, wakiwa 16,582, wakifuatiwa na wanawake 15,412, wazee 789 na watu wenye ulemavu 741.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!