Wakati taifa la Ufarasa leo likiazimisha Sikukuu ya kitamaduni inayo fanyika kila mwaka tarehe 31 Oktoba ambapo ni mkesha wa kuamkia sikukuu ya Kikristo inayo tajwa kuwa ni Siku ya Watakatifu Wote inayoadhimishwa Novemba 1.
Taifa hilo linatajwa kukabiliwa na wimbi kubwa la machafuko mapya ya kitaifa huku serikali ya Rais Emmanuel Macron ikionya kuchukua hatua kali za kisheria na kiusalama kudhibiti ghasia zinazoendelea kutikisa nchi hiyo.
Hali hii imeripotiwa leo Oktoba 31,2026 kufuatia maandamano yanayofanyika Jumamosi hii nchini humo huku ikiwa ni wiki ya tatu mfululizo ya mapambano ya mitaani, yakisukumwa na msimamo mkali wa waandamanaji wanaohisi kuwa ahadi za awali za serikali za kurekebisha sekta ya elimu na kupunguza gharama za nishati zimeshindwa kabisa kutatua matatizo yao ya msingi.