Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuzindua Kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, toleo la mwaka 2026, kesho Novemba 18, 2026, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Pwani

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo novemba 17, 2026 kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema sambamba na uzinduzi wa kitambulisho hicho, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) itazindua rasmi huduma mpya inayojulikana kama ‘Huduma Bila Foleni’ inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma, kupunguza muda wa wananchi kusubiri na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za mamlaka hiyo.
Nyongo amezitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na usajili wa wananchi ambao bado hawajasajiliwa katika mfumo wa NIDA, uhakiki na marekebisho ya taarifa za utambulisho, ufuatiliaji wa hatua za maombi ya vitambulisho vya Taifa pamoja na utoaji wa vitambulisho kwa wananchi wenye namba za utambulisho wa Taifa ambao bado hawajavichukua.
Baada uzinduzi huo katika viwanja vya stendi ya zamani maili moja, Waziri Mkuu atafanya mkutano wadhara na wananchi, na viwanja katika siku ya pili ya ziara hiyo, Novemba 21, 2026, Waziri Mkuu atatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ambako pia atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Polisi Chalinze.