Latest Posts

BAVICHA KANDA YA VICTORIA WALAANI MWENDELEZO WA MATUKIO YA WATU KUTEKWA

Theophilida Felician, Kagera.

Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA (BAVICHA) Kanda ya Victoria limelaani na kukemea matukio ya watu kutekwa yanayoendelea kujitokeza nchini.

Akitoa kauli hiyo, tarehe 19 Februari 2025 Mwenyekiti wa BAVICHA Kanda, Fred Michael akiwa kwenye kikao cha baraza hilo Jimbo la Bukoba Mjini amesema kumekuwepo mwendelezo wa matukio ya watu hususani WanaCHADEMA kutekwa na wengine kupoteza maisha, akigusia tukio la karibuni la kutekwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza Amani Mohamed Manengelo.

Fred amesema wao kama baraza wanalaani matukio hayo huku wakitoa maagizo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Innocent Bashungwa na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi kubaini waliko watu wanaotekwa.

Aidha amerejea kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Burhan aliyoitoa mwaka 2024 yenye kusema kuwa ‘watakaomtukana Rais wakipotezwa wasiwatafute’, kauli ambayo amesema inawapa machungu ukilinganisha na hali ya utekaji inayoendelea kujitokeza.

Kutokana na hilo, ametoa maagizo kwa Waziri Bashungwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera kumchukulia hatua za kisheria Burhan dhidi ya kauli yake hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!