Latest Posts

BILIONI 40.873 ZABORESHA UWANJA WA NDEGE WA SONGEA

Waziri wa Ujenzi wa Tanzania Innocent Bashungwa amesema kuwa serikali ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa bilioni 40.873 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa ya uwanja wa ndege wa Songea ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100.

Bashungwa ameyasema hayo siku ya Jumatatu Septemba 23, 2024 wakati Rais Samia alipowasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma, ambapo amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uwanja huo, Wanaruvuma wanaweza kusafiri maeneo mbalimbali ya nchi kwani ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) huwasili uwanjani hapo mara tatu kwa wiki.

Amesema ujenzi wa uwanja huo umefanikiwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Ujenzi

“Mheshimiwa Rais Wizara tunakushukuru sana kwa ‘mabilioni’ haya ambayo umetupatia sasa tunaona pamoja na kazi nzuri ambayo inaendelea ya ujenzi wa barabara za kuunganisha mkoa wa Ruvuma, lakini serikali unayoiongoza ya awamu ya sita imewawezesha Wanaruvuma kuweza kupata usafiri wa uhakika wa ndege ambazo zinakuja hapa mara tatu”, Amesema Bashungwa.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanja hicho Dustan Komba amesema maeneo yaliyoboreshwa ni pamoja na njia ya kutua na kurukia ndege na kutoka urefu wa mita 1600 kwenda mita 1860, usimikaji wa taa za kuongozea ndege kwa ajili ya kuwezesha ndege kutua saa 24.

Maboresho mengine ni pamoja na kituo cha kupokea nishati kwa maana ya maji na umeme, katika line ya umeme yenye msongo wa kilowati 33 na lami ambayo inakidhi viwango na vigezo  na yenye miundombinu  toshelevu kwa ajili ya utuaji wa ndege.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!