Latest Posts

DC MPOGOLO ATOA NENO MARAIS 54 KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII ILALA KATIKA MKUTANO WA AFRIKA WA NISHATI SAFI

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha diplomasia ya kimataifa, hali inayodhihirishwa na ugeni wa Marais 54 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

DC Mpogolo alitoa pongezi hizo kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), wakati akizungumzia maandalizi ya Mkutano wa Afrika wa Nishati Safi unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi 28, 2025.

Katika mahojiano hayo, Mpogolo alitaja vivutio vya kipekee vya utalii vilivyopo Wilaya ya Ilala ambavyo wageni wa mkutano huo watatembelea. Miongoni mwa vivutio hivyo ni Soko la Samaki Feri, nyumba ya kihistoria ya wakoloni inayojulikana kama Ngome, na kumbi mbili za kihistoria za mikutano, Karimjee na Anatoglo. Aliongeza kuwa vivutio vingine ni sehemu za mapumziko zinazochangia uzuri wa eneo hilo.

Aidha, Mpogolo amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya mkutano huo kimkakati kutangaza bidhaa na huduma zao kwa wageni wa kitaifa na kimataifa watakaohudhuria. “Huu ni wakati muhimu kwa wafanyabiashara wetu kuonyesha bidhaa zao kwa hadhira kubwa kutoka sehemu mbalimbali za dunia,” alisisitiza.

Kuhusu maandalizi ya mazingira, DC Mpogolo alieleza kuwa Wilaya ya Ilala inaendelea na kampeni ya usafi kwa lengo la kuhakikisha wageni wanakaribishwa katika mazingira safi na yenye mandhari ya kuvutia.

Mkutano huo wa Afrika wa Nishati Safi unatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kujadili mikakati ya kukuza nishati mbadala kwa maendeleo endelevu barani Afrika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!