Latest Posts

DIT MWANZA YAIMARISHA MIUNDOMBINU, SERIKALI YAIPONGEZA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi amepongeza juhudi zinazofanywa kupokea wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita katika Taasisi ya Teknolojia Dae es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza unapojengwa mradi wa kujenga ujuzi kwa maendeleo na uingiliano wa kikanda Afrika Mashariki (EASTRIP)

Profesa Mushi ametoa pongezi hizo mara baada ya kuutembelea mradi huo wa EASTRIP unaogharimu shilingi bilioni 37 fedha kutoka benki ya dunia na baada ya kukamilika utakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi 2,000 kutoka 200 wa sasa

“Kutokana na mpango wa serikali wa elimu bila ada, idadi ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita inaongezeka.Tunahimiza elimu ya amali ambayo inapatikana vyuo kama hivi.  Sasa mkandarasi aongeze bidii kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa,”

Kaimu Mkurugenzi wa Kampasi, Eng. Issa Mwanagosi, amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 70 na unatarajia kukamilika Agost mwaka huu, kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa mwaka ujao wa masomo

Mwangozi ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine, mradi unahusisha ujenzi wa jengo la taaluma, la utawala, mabweni mawili, pamoja na karakana ya kuchakata Ngozi huku baadhi ya miundombinu imeanza kutumika kama vile madarasa a baadhi ya ofisi

Kukamilika kwa mradi huo wa EASTRIP kwenye kampasi ya DIT Mwanza kunatajwa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira nchini kwa wanafunzi kupata ujuzi wa namna ya kutengeneza bidhaa za ngozi na kuziuza hali itakayosaidia kujiongezea kipato chao na nchi kwa ujumla

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!