Latest Posts

DOROTHY: ACT HAITOSUSIA UCHAGUZI, ITAPAMBANIA DEMOKRASIA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Jonas Semu, amesema mwaka 2025 si mwaka wa kawaida kwa chama hicho, bali ni mwaka wa kipekee unaohitaji uongozi madhubuti katika kupigania demokrasia na kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao.

Akizungumza Jumatatu kwenye maadhimisho ya miaka 11 ya kuzaliwa kwa chama hicho, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo Makao Makuu ya ACT, Dar es Salaam, Dorothy amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi kwa makusudi na dhamira ya dhati.

“Kama nilivyotangulia kusema kwenye salamu zangu, huu sio mwaka wa kawaida kwetu, ni mwaka wa kipekee… chama chetu kitapambana kikishiriki na kitashiriki kikipambana,” amesema Dorothy.

Dorothy amesema uamuzi wa ACT kushiriki uchaguzi haukuja kwa bahati mbaya, bali umetokana na tafakuri ya kina na uchambuzi wa hali ya kisiasa nchini.

“Sababu zetu ni tatu: Mosi, tumejiridhisha tunashiriki kulinda thamani ya kura. Pili, tumejiridhisha kuwa kususia uchaguzi kunaimarisha udikteta. ACT Wazalendo tukisusia, CCM itafurahia. Tatu, CCM imeshindwa kuendesha nchi, ikae pembeni, tutaishinda,” ameeleza Dorothy.

Amesisitiza kuwa mbali na jukumu la kisiasa la kushiriki uchaguzi, ACT Wazalendo ina wajibu mkubwa wa kitaifa wa kuongoza mapambano ya kulinda na kutetea demokrasia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!