Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kuhakikisha ujenzi wa miundombinu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kahimba iliyopo wilayani humo unakamilika kwa wakati ili kuruhusu kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ifikapo Januari 13, 2025.
Rugwa ametoa maelekezo hayo alipotembelea na kukagua maedeleo ujenzi wa Shule hiyo sambamba na kujionea maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kwa Mwaka 2025 kwa shule hiyo.
Aidha Katibu Tawala amemsisitiza Mkurugenzi huyo kuhakikisha anawaelekeza wakandarasi kuongeza idadi ya mafundi ili kukamilisha kazi zinazotakiwa kufanyika kwa wakati.
Aidha Rugwa amemsisitiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo George Mbilinyi kutosita kuwachukulia hatua wakandarasi watakaoshindwa kutekeleza matakwa ya mikataba yao inayohusiana na ujenzi wa shule hiyo.