Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo amewataka maafisa usafirishaji kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika mikakti yake ya kuendelea kukuza uchumi wa nchi.
Mpogolo amesema hayo katika mkutano wa kuliombea taifa uliofanyika wilayani Ilala na kuhudhuriwa na viongozi wa dini wa imani zote.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mpogolo ameungana na maafisa usafirishaji na viongozi dini katika dua hiyo na kueleza mapenzi ya maafisa usafirishaji kwa kumuunga mkono Rais Dkt Samia kwa kumchangia fedha za kuchukua fomu ya Urais mwaka huu 2025.
Amesema kitendo cha kushiriki katika maombi ya dua kwa taifa, kumuombea kiongozi huyo na kuuombea uchaguzi Mkuu kuwa na amani ni uzalendo kwa taifa lao.
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wa dini na maafisa usafirishaji kwa kushiriki katika maombi hayo ya kuiombea nchi amani.
Kwa upande wa viongozi wa dini wameonesha upendo, mshikamano na kielelezo cha mwaka 2025 kuwa mwaka wa amani katika uchaguzi.
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa 4R za Rais Dkt Samia, kwa maafisa hao na Watanzania ambazo Rais ameendelea kuzitumia ambazo ni maridhiano, mabadiliko, ustamilivu na kuijenga nchi kwani kipindi cha nyuma walikua hawaingii mjini jambo ambalo 4R imehakikisha wanaingia ili kuendesha maisha yao.
Akijibu risala ya maafisa usafirishaji kuhusu kadhia ya upatikanaji leseni, Mpogolo amewahakikishia kukutana na Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili leseni zipatikane.
Kuhusu suala la maombi ya vituo kwa maafisa usafirishaji, DC Mpogolo, amesema bado serikali inaendelea kuwasikiliza na kuwataka maafisa hao wafuate utaratibu.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na maafisa usafirishaji ili waweze kufanya kazi zao vizuri ikiwa ni pamoja na ongezeko la vituo kutokana na maombi yao bodaboda na bajaji.