Na Helena Magabe-Tarime
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mara (MRPC) Jacob Mugini awatataka waandishi wa habari Wanawake wa Mkoa wa Mara kuachana na majungu na badala yake wafanye kazi kwa bidii kwa kukijenga chama na kufanya maendeleo katika Jamii ili kuweka kumbukumbu nzuri kwa vizazi vijavyo.
Mugini ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari waanawake Mkoa wa Mara kilichofanyika jana juni 3,2025 katika ukumbi wa Hotel ya Goldland Tarime mjini aliwaasa waandishi hao kuachana na majungu na baadala yake wafanye kazi kwa bidii wakijenge chama kwaajili ya vizazi vijavyo ili hata watoto wao wa kike watakapo bahatika kuwa waandishi wajifunie wazazi wao kuwa waanzilishi wa chama hicho.

Alisema chama hicho ni taasisi kubwa endapo waandishi kwa pamoja watafanya kazi bila majungu itakuwa kubwa na yenye mafanikio itaheshimika na yenye kukubalika kwenye jamii kwani itakuwa rahisi kuwavuta watu na kuongeza kuwa Mtu asiposemwa ni kama jiwe lakini tu hivyo kusenwa ni lazima aidha kwa mazuri au kwa mabaya ambapo alisema yeye mtu akimsema vibaya hamsemi bali anaepukana naye na kujitenga nae na maisha yanaendelea.
kwa kuvutiwa na jina cha chama cha waandishi wa habari Wanawake wenye maono( Visionary Womens Journalist) alitoa kifupi cha jina la chama hicho kuwa litakuwa VWJ na akasema kuwa wanaweza kuluka W na kujiita wana VJ ambapo aliahidi kuwatengenezea nembo (logo) nzuri ya chama itajayokuwa inatumika vile vile na kwenye tishert zao .
Mbali na hilo aliahidi kuwaingiza wanachama wote 15 NSSF na kuwataka kuwa wabunifu wa kuomba miradi na tenda mbali mbali ili kujiingizia pesa ambazo kwa baadae wanatakiwa kugawana kwa usawa,miradi aliyoitaja ni pamoja na kuomba tenda za usafi,kupamba,kupika, kuwa na viti vya kukondisha na kusisitiza kulinda tasisi hiyo isichafuke bali iwe ya kuheshimika na kukubalika kwenye Jamii.