Latest Posts

MTENGA AMUOMBA DMO WA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI KUJIPANGA KUTOKOMEZA MALARIA

Katika kipindi cha mwaka 2024 maambukizi ya Vimelea vya Malaria ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara ni asilimia 8.9 kutoka asilimia 7.2 kwa mwaka 2023 ikiashiria kuongezeka kwa maambukizi katika manispaa hiyo.

Jumla ya wagonjwa 654 kati ya 124,059 ya waliolazwa katika mwaka huo 2024 walikuwa na ugonjwa wa malaria na jumla ya wagonjwa 13,352 kati ya 230,017 ya wagonjwa wote wa nje walibainika kuwa na vimelea vya maralia sawa na asilimia 5.8

Hayo ameyaeleza Mratibu wa Malaria wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Charles Mgaya wakati wa kupokea Chandarua 200 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga.

Ameongeza kuwa Manispaa hiyo ina uwepo wa mazalia ya mbu ya kudumu 11 yanayozalisha kiasi kikubwa cha mbu ambapo zinahitajika takribani ya lita 800 za viuadudu vya kibaorojia zinazo gharimu kiasi cha shilingi 10,600,000 ili kutekeleza zoezi la unyunyizi kikamilifu na kupunguza kiasi cha mbu waenezao malaria.

Hata hivyo Manispaa hiyo imeomba wadau mbalimbali wa afya na  jamii kuhamasisha matumizi ya vyandarua vyenye viuatilifu kila siku, kufanya usafi wa mazingira na matumizi ya chanjo ya malaria kwa wajawazito na kuwahi vituo vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake Katibu Mwenezi Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mtwara mjini Mohamed Watanga amewataka wananchi kutumia vyandarua ili kulinda afya zao na wasitumie kwaajili ya kufugia kuku ambapo amesema wapo baadhi ya wananchi wanatumia vyandarua kwa ajili ya ufugaji na sio kwenye kujikinga na malaria.

“Kuna kawaida mtu unachana neti unazungusha  unaweka vifaranga,hiko kifaranga hakitokuwa na faida kama afya yako imeteteleka, niwaombe tukatumie neti kwa makusudi yaliyokusudiwa.”Amesema Watanga

Mbunge wa Jimbo hilo la Mtwara mjini Hassan Mtenga amesema mkoa huo ni nafasi ya pili nchi nzima kwa ukuaji wa Malaria hivyo amemuomba Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo kuandaa programu kwa ajili ya kuufanya mji huo kuwa msafi ili kupunguza mazalia ya mbu.

“Niwaombe wenyeviti wa mitaa waweke mipango mikakati kwa ajili ya kudhibiti malaria kwa kuhamasisha wananchi kufanya usafi kila nyumba”Amesema Mtenga

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!