Latest Posts

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TEMEKE AAGIZA LAPTOP ALIZOZIGAWA ZIKAJAZE KURA ZA SAMIA

.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke Ndugu Hamisi Slim  Septemba 222024 amegawa komputa mpakato (Laptop) kwa kila Katibu Kata wa Jumuiya ya Wazazi kwa Wilaya nzima ya Temeke yenye Kata 23 zenye thamani ya shilingi milioni kumi na mbili (12000000)

Ndugu Slim amegawa Laptop hizo katika Kikao cha Baraza la Kikanuni Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Temeke sambamba na kutoa vyeti kwa Kata zilizofanya vizuri katika usajili wa Wanachama wa Jumuiya hiyo ambapo Kata ya Chamazi imeongoza kwenye usajili huo.

“Laptop hizi ni si mali ya mtu ni mali ya Jumuiya na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla, ziende zikasaidie kutafuta kura za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Chama cha CCM kwa ujumla” .Alisema Ndugu Slim.

Awali Baraza hilo lilifunguliwa na Ndugu. Dkt. Ibrahim Msengi (MNEC) na kufungwa na Ndugu Khadija Ally Said Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar-es-Salaam.

Kwa upande wake Bi. Khadija amewaambia Wajumbe wa Baraza waende wakafanye kazi kwenye Kata zao kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinashika dola.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!