Latest Posts

MZEE MAGABE- WAKULIMA WAZEE WA BARA WALIPWE PENSHENI KAMA WA ZANZIBAR

Mkulima na mfugaji ambaye ni mwenyekiti mstaaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mtaa wa Kogete kata ya Kenyamonyori, wilayani Tarime mkoani Mara, Anicet Gasper Magabe ameiomba serikali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kuwalipa pesheni wakulima wazee wa Tanzania bara kama wanavyolipwa wazee wa Tanzania visiwani.

Akizungumza na Jambo TV, Magabe amesema vyanzo vya mapato vya Tanzania bara ni vingi kuliko Tanzania visiwani (Zanzibar) lakini wazee wa bara hawalipwi hivyo ameiomba serikali kuwalipa wazee wakulima wa jinsi zote kwani makundi yote yamekumbukwa isipokuwa wakulima.

Amesema wakulima wengi hawana uwezo wa kujilipia bima za afya na pindi wanapokuwa wazee hupata changamoto ya matibabu kwani wengi wao hawana uwezo wa kusomesha watoto ambao wangeweza kuwakatia bima hivyo wakatapokuwa katika hali ya kujiweza kiuchumi.

“Kama serikali labda itaona miaka 60 wazee watakuwa wengi basi inaweza kusogeza hadi miaka 70 kupitia Dira ya Taifa ya miaka 50 wafanye namna wazee wengine wasipitie shida kama tulizopitia. Sisi Zanzibar wanalipwa laki moja na nilisikia wanataka kuboreshewa, mzee ukipata laki moja kila mwezi ni hela nzuri itakusaidia”, amesema Anicet.

Kwa upande mwingine ameongelea soko duni la zao la mahindi pindi yanapovunwa bei hushuka kiasi cha kukatisha tamaa hivyo ameomba serikali inapowahimiza wananchi kulima iwatafutie na soko la uhakika ili wasipate hasara kwani wanatumia gharama kubwa, lakini wakati wa kuuza bei inashuka na walanguzi wanatumia madebe ya lumbesa yanayowapa hasara wakulima.

Aidha ameomba bei ya kahawa kwa kilo kama kuna uwezekano wa kuongeza hadi angalau 4000 ongezeke kama ilivyo kwa Bukoba ambapo msimu ulioisha waliuza kilo kwa shilingi 5000 lakini Tarime waliuza kilo kwa shilingi 3000.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!