Latest Posts

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AHIMIZA UWEKEZAJI KATIKA TEKNOLOJIA YA AI KWA MAENDELEO ENDELEVU

Wito umetolewa kwa sekta binafsi, taasisi za elimu, na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kuhakikisha maandalizi bora ya vizazi vijavyo kwa ajili ya uchumi wa akili bandia au Akili Mnemba (Artificial Intelligence – AI).

Wito huo umetolewa Septemba 26, 2024, jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipokuwa akifungua mkutano wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT).

“Tunahitaji kuwekeza katika mafunzo ya kitaaluma na kujenga uwezo wa wafanyakazi wetu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na nafasi nzuri ya kufaidika na mapinduzi haya ya kidijiti,” amesema Mhandisi Mahundi.

Mhandisi Mahundi amesema serikali iko tayari kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha matumizi bora ya teknolojia za AI yanatumika kuboresha maisha ya Watanzania na kuimarisha uchumi wa nchi.

“Kwa pamoja, tunaweza kufanya mabadiliko haya ya kidijiti kuwa kichocheo cha maendeleo endelevu na ustawi wa taifa letu. Ni matumaini yangu kuwa matokeo ya mkutano wa leo yatasaidia kuweka msingi imara wa uongozi wa kidijitali nchini”, amesema Mahundi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!