Latest Posts

NYALANDU AWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO KULIENDESHA TAIFA

Na Josea Sinkala, Mbeya.
 
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania wakati wa serikali ya awamu ya nne Lazaro Nyalandu, amewataka vijana nchini kujiamini kwani ndio tegemeo la Taifa kwa kizazi cha sasa na baadaye.
 
Nyalandu ametoa wito huo wakati akizungumzia kongamano la mtandao wa vijana (Vijana na Tanzania) linalotarajiwa kufanyika jumapili hii (Oktoba 20, 2024) jijini Mbeya lenye lengo la kuwaelimisha vijana juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu kwa ajili ya Taifa.
 
Miongoni mwa makusudi ya kuwajengea vijana nchini ni juu ya uzalendo na kile watakacholifanyia Taifa lao.
 
Nyalandu amesema vijana ndio wenye hatma ya Taifa ambalo limedumu katika amani na mshkamano hivyo kuwataka kuendelea kuwa raia wema kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.
 
Pia ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwaamini vijana katika maeneo mbalimbali na kuwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii, weledi, uzalendo na malengo endelevu ya taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!