Latest Posts

RC MARA AAGIZA WATOA HUDUMA WANDANI KULIPWA KWA WAKATI

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amepiga marufuku kwa halmashauri kuacha kukopa na kulimbikiza madeni kwa watoa huduma wa ndani kwani kufanya hivyo nikuzorotesha mitaji na ukuaji wa uchumi wao.

Kanali Mtambi ametoa kauli hiyo wakati wa kujadili utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Mtambi amesema ni vyema halmashauri zikahakikisha kwenye mapato yao zinatenga na kuwalipa kwa wakati watoa huduma badala ya kukaa na fedha zao miaka na miaka na kupelekea kudumaza biashara zao.

“Madiwani hakikisheni mnasimamia mipango na bajeti yenu kwa Halmashauri na mhakikishe makusanyo yenu miongoni mwa kipaumbele ni kuwalipa watoa huduma wetu, hususani wa ndani kwa kumkuza yule ndio unakuza uchumi lakini kama ukimporomosha na wewe Halmashauri ndio unajiua”, amesema Kanali Mtambi.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!