Latest Posts

SHERIA ZA MAZINGIRA ZAZAA MATUNDA KWA WACHIMBAJI WADOGO GEITA

Serikali imeendelea kusisitiza umuhimu wa wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia utunzaji na uhifadhi wa mazingira wanapotekeleza shughuli zao. Katika wilaya ya Geita, baadhi ya migodi midogo, ikiwemo wa Ushirika wa Mgusu na ule unaomilikiwa na Rajabu Seif, imekuwa mfano bora wa utunzaji wa mazingira kwa kuhifadhi uoto wa asili.

Mtandao huu umetembelea migodi hiyo na kushuhudia uoto wa asili ukiwa umestawi vyema, huku mimea ikiwa imetunzwa bila kuharibiwa, jambo linaloonyesha juhudi kubwa za wachimbaji katika kulinda mazingira.

Erick Joseph, mwakilishi wa wanachama wa mgodi wa Mgusu, ameeleza kuwa walipofika kuanza shughuli za uchimbaji, walikuta maeneo yakiwa yameharibika, lakini waliweka mikakati ya kurejesha hali ya mazingira kwa kupanda miti na kuhifadhi uoto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Ushirika wa Mgusu, Modest Masabile, amesema hatua yao ya kufanikisha utunzaji mazingira inatokana na kufuata sheria walizopatiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Naye Rajabu Seif, mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu wilayani Geita, ameainisha mikakati waliyoweka katika eneo lake la mgodi ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa ipasavyo.

Kwa upande mwingine, Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Abert Hausoni, amesema wachimbaji wadogo wanapaswa kutumia miti kutoka kwa wasambazaji waliosajiliwa ili kuepuka ukataji miti kiholela unaoharibu mazingira.

Juhudi hizi zinaonesha mwamko mpya kwa wachimbaji wadogo katika kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa kuzingatia misingi ya uhifadhi wa mazingira, sambamba na kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!