Latest Posts

SWIFPACK: HUDUMA YA KIDIGITALI ITAKAYOBORESHA USAFIRISHAJI NA AJIRA TANZANIA

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa Elia Madulesi ametoa wito kwa Watanzania na wamiliki wa vyombo vya moto kuchangamkia fursa ya huduma ya usafirishaji ya SwifPack, itayokwenda kuwa mwarobaini ya changamoto ya ajira nchini hasa kwa kundi la vijana.

Ametoa kauli hiyo Januari 21, 2025 Jijini Dar es salaam ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kuelekea uzinduzi wa huduma hiyo muhimu Januari 23 mwaka huu ambapo itatoa huduma za usafirishaji kuanzia bodaboda hadi magari ya tani 30.

“Sisi tulivyojipanga ni kuhakikisha madereva wanapata manufaa ya kufanya hii kazi ndio maana tunasema ni fursa ya ajira tunaposema fursa ya ajira maana yake tumeenda kwenye eneo pana zaidi, kuhudumia watu wengi zaidi kwa mtazamo mpana zaidi ndo maana tunasema SwifPack imekuja na majibu ya maswali ambayo huduma zingine zilizo tangulia hazikuweza kujibu” amesema Madulesi

Amesema tofauti ya huduma ya SwifPack na huduma zingine za usafiri wa kidigitali ni kuwa yenyewe itakuwa mikoa yote nchi nzima Tanzania bara na Visiwani Zanzibar, mijini na vijijini hivyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa kurahisisha sekta ya usafirishaji.

Ameeleza namna ambavyo huduma hiyo ya kidigitali itawanufaisha moja kwa moja wananchi ni kupitia madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri kusajili vyombo hivyo, na kuanza kutoa huduma kwa jamii, ambapo mtumiaji atapakua programu ya Swifpack na kuitumia kupitia simu ya mkononi mahali popote.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kwa ujumla kutumia fursa hiyo ambayo ni mkombozi kwasababu mbali na kwakuwa imeenea nchi nzima, haitoi ajira kwa vijana waliopo mijini pekee bali kwa waliopo nje ya miji na sehemu zilizo sahaulika.

Amesema pia huduma hiyo itakuwa tofauti na huduma za usafirishaji kidigitali zilizotangulia kwamba itaenda kuwa mkombozi wa watangulizi hao na kuziba pengo kwasababu itakuwa inapatikana kwa haraka, urahisi na usalama, pia mtumiaji anaweza kufuatilia kifurushi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!