Latest Posts

TISHIO LA TRUMP: VIONGOZI WA EU WAKUTANA BRUSSELS KUJADILI USALAMA WA BARA HILO

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Brussels siku ya Alhamisi kwa mashauriano maalum kuhusu ulinzi wa bara hilo, huku Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, akitaja hali ya sasa kama “mabadiliko ya kihistoria.”

Mkutano huu unafanyika wakati Umoja wa Ulaya ukitathmini jinsi unavyoweza kuiunga mkono zaidi Ukraine, kufuatia tangazo la Rais wa Marekani, Donald Trump, la kusitisha misaada kwa Kyiv.

Katika mkutano huu, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amealikwa kushiriki, wakati wasiwasi kuhusu usalama wa bara hilo ukizidi kuongezeka tangu mvutano kati yake na Trump uliotokea Ikulu ya White House wiki iliyopita.

Hatua za utawala wa Trump, pamoja na msimamo wake wa kirafiki kwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, zimewaacha viongozi wengi wa Ulaya wakiwa na mashaka kuhusu ikiwa bara hilo linaweza kutegemea tena msaada wa Marekani katika masuala ya ulinzi.

Uamuzi wa Washington siku ya Jumatano wa kusitisha ushirikiano wa kijasusi na Ukraine umeongeza hofu zaidi, huku mataifa ya Ulaya yakiharakisha kutafuta njia mbadala za kujilinda. Rais Macron, akijibu wasiwasi huu, amesema Ufaransa iko tayari kujadili upanuzi wa ulinzi wake wa nyuklia kwa washirika wa Ulaya, hatua ambayo inazua mjadala mpya kuhusu mustakabali wa usalama wa bara hilo.

Wito huo umeungwa mkono na Friedrich Merz, anayeonekana kuwa mgombea mwenye nafasi kubwa kuwa Kansela ajaye wa Ujerumani, ambaye amependekeza kujadili uwezekano wa kuongeza kwa ugavi wa silaha za nyuklia kwa usalama wa Ulaya.

Katika juhudi za kuimarisha ulinzi, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) imepewa ruhusa ya kufadhili miradi ya kijeshi, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa bara hilo katika kujitegemea kijeshi. Rais Macron amepanga kuandaa mkutano wa wakuu wa majeshi ya Ulaya jijini Paris wiki ijayo, ambapo mipango zaidi ya kuimarisha ulinzi wa bara hilo itajadiliwa.

Macron ameweka wazi kuwa, hatua madhubuti zitachukuliwa mjini Brussels ili kuzifanya nchi za Ulaya kuwa “tayari zaidi kujilinda.” Akihitimisha hotuba yake, amesisitiza kuwa “Wakati huu tunahitaji maamuzi ambayo hayajawahi kufanywa.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!