Latest Posts

TUZO ZA WATENDAJI WAKUU BORA 100 ZA MWAKA 2024 ZASISITIZA UONGOZI NA UBUNIFU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Sharif Ali Sharif, ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania kubuni miradi inayoendana na sera za uwekezaji nchini, akisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa kwa vitendo.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Watendaji Wakuu Bora 100 wa Mwaka 2024 zilizofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Sharif amesema Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo vijana wanapaswa kuyatumia kwa ajili ya kukuza kampuni zao na kuzitangaza kwenye masoko ya ndani na nje.

Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Kampuni ya Eastern Star kwa kushirikiana na The Global CEO Institute, ilikusanya viongozi waandamizi wa taasisi na kampuni mbalimbali zilizofanya vizuri mwaka huu.

Mkurugenzi wa Eastern Star, Bw. Deogratius Kilawe, amesema lengo la tuzo hizo ni kusherehekea uongozi bora, kuhimiza uvumbuzi, na kuhamasisha kizazi kijacho cha watendaji.

Baadhi ya washindi wa tuzo hizo wameeleza kuwa ushindi wao ni motisha ya kuendelea kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi mahitaji ya soko la kimataifa, huku wakisisitiza umuhimu wa kuweka mkazo kwenye ubora na uvumbuzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!