Latest Posts

UFAULU KIDATO CHA NNE WAPANDA, WENGINE WAFUTIWA KWA KUANDIKA MATUSI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Said Mohammed, ametangaza kuongezeka kwa ufaulu wa mitihani ya kidato cha nne mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2023.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza matokeo hayo, Dkt. Mohammed alisema kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 3, na kufikia asilimia 92.37. Hii inamaanisha kuwa watahiniwa 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne (Div I-IV).

“Mwaka 2023, watahiniwa waliofaulu walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36. Hii inaonyesha ongezeko kubwa la ufaulu kwa mwaka huu wa 2024,” amesema Dkt. Mohammed.

Dkt. Mohammed ameongeza kuwa ufaulu kwa watahiniwa waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu (Div I-III) umeongezeka kwa asilimia 5.54 ikilinganishwa na mwaka 2023.

“Watahiniwa wa shule waliopata ubora wa ufaulu katika madaraja ya I-III ni 221,953 sawa na asilimia 42.96. Mwaka 2023, idadi hiyo ilikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.42,” amesema Dkt. Mohammed, akisisitiza kuwa ongezeko hilo linaashiria juhudi za maboresho katika sekta ya elimu.

Dkt. Mohammed amesema kuwa takwimu hizi zinaonesha maendeleo chanya katika elimu nchini, huku akitoa pongezi kwa walimu, wazazi, na wanafunzi kwa juhudi zao katika kufanikisha matokeo mazuri.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!