Latest Posts

VIONGOZI WA UPINZANIA WAOMBA CHAGUZI ZIJAZO ZIWE ZA HAKI

Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wameomba uchaguzi uwe wa uwazi na wahaki ili kudumisha amani iliyopo kwenye maeneo yao.
Hayo yamebainishwa mara baada ya kutolewa maelekezo ya uchaguzi Septemba 26,2024 na Msimamizi mkuu wa uchaguzi Mhandisi Mshamu Ally Munde kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA halmashauri ya mji Nanyamba Shabani Ally amesema uchaguzi uliopita ulikuwa na changamoto mbalimbali hadi kupelekea baadhi ya vyama kujiondoa katika uchaguzi ingawa kwa mwaka huu dalili njema zimeshaanza kuonekana kuendelea kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza kwenye kikao hicho cha maelekezo ya uchaguzi msimamizi mkuu wa uchaguzi Mhandisi Mshamu Ally Munde amewataka wakazi wa halmashauri hiyo kushiriki kikamilifu kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura hadi kuwania nafasi za uongozi kwani ni haki ya kila mtanzania.
Aidha amewataka wagombea wa vyama vya siasa kuendesha kampeni zao kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kwa kuzingatia muda kuepuka yale yote yaliokatazwa kama vile kutumia rushwa,lugha zisizofaa na ubaguzi wa namna yoyote ile.
Ameongeza kuwa uchaguzi utakuwa wa haki,usawa na uwazi na kuwahakikishia kuwa changamoto zote ambazo zilijitokeza chaguzi zilizopita zimeshafanyiwa kazi na hazitajitokeza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!