Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Gairo Dunstan Mwendi amesema serikali ya wilaya hiyo imejipanga kukabiliana na wale ambao watajaribu kuharibu miundombinu ya maji hasa wanaokata mabomba.
Mwendi ameyasema hayo Jumanne Juni 11, 2024, wakati akikabidhi mabomba ya maji ambayo yameelezwa kuwa yanaenda kutatua changamoto ya maji katika wilaya ya Gairo ambapo amesisitiza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua kali wale ambao watadiriki kuharibu miundombinu hiyo.
Pia, Mwendi ameongeza kuwa serikali inafanya kazi kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya miundombinu ya maji ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama.