Latest Posts

WANANCHI NA WADAU MTWARA WAOMBA ELIMU ZAIDI KUHUSU NYANGUMI FESTIVAL

Baadhi ya wananchi na wadau mbalimbali mkoani Mtwara wamewaomba waandaaji wa Tamashha la Nyangumi Festival kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa wananchi kushiriki katika maonyesho hayo, sambamba na kuwahamasisha wakaazi wa maeneo husika kutumia fursa zinazopatikana kupitia tamasha hilo kwa ajili ya kufanya biashara.

Wakizungumza katika Tamasha la Nyangumi Festival lililofanyika katika Kijiji cha Msimbati, Kata ya Msimbati, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wananchi hao wamesema kuna umuhimu wa jamii kupewa elimu ya kutosha ili iweze kutambua fursa zinazotokana na sekta ya utalii na bahari.

Mmoja wa wadau, Grace Tendesi, ameshauri waandaaji wa tamasha hilo kuongeza utoaji wa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu umuhimu wa utalii wa baharini na namna wanavyoweza kunufaika na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kutoa maelekezo kwa taasisi mbalimbali kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika Tamasha la Nyangumi Festival, kama ambavyo zinavyoshiriki katika matukio mengine yanayofanyika mkoani humo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi amesema uongozi wa mkoa umechukulia tamasha hilo kwa uzito mkubwa, huku akiwataka wadau mbalimbali kujitokeza na kutumia fursa zilizopo, ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya utalii.

Aidha, Mdhamini wa Mradi wa Tuhifadhi Bahari Yetu Project, Remmy Lema, amesema kupitia jukwaa la Nyangumi Festival wamefanikiwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha shughuli zinazofanywa kwenye sekta ya utalii.

Amesema ushirikiano huo pia umesaidia katika kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira ya bahari na kupunguza uharibifu wa maeneo ya utalii, hatua inayolenga kuhakikisha rasilimali hizo zinaendelea kuwepo na kunufaisha kizazi cha sasa na kijacho.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!