Latest Posts

WAZAZI WATAKIWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

Wazazi na walezi wametakiwa kujitoa kwa dhati katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao, ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, badala ya kutegemea Serikali pekee.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mwatulole, Mussa Makomiane, yaliyofanyika katika Kata ya Buhalabahala, Wilayani Geita.

Makumiane amesema ushirikiano kati ya Serikali, wazazi, walezi na wadau wa maendeleo ni muhimu katika kuboresha mazingira ya elimu na maendeleo kwa ujumla, akiwataka wananchi kutumia fursa walizonazo kuchangia maendeleo ya jamii zao.

Katika taarifa ya wahitimu wa kidato  cha nne  ambayo imesomwa na Diana Mapambano   wamemuomba mgeni rasmi   Makumiane, ambaye ni mdau wa maendeleo ya elimu nchini, kusaidia kukamilisha ujenzi wa uzio wa shule hiyo, ikiwa ni hatua ya kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali za shule.

Akijibu ombi hilo, Makumiane ametoa msaada wa mifuko 50 ya saruji pamoja na mchanga wa tipa tatu, kwa ajili ya kusaidia kukamilisha ujenzi wa uzio huo.

Aidha, amewahimiza wazazi na walezi kuendelea kushirikiana na shule pamoja na Serikali kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia na kufikia malengo yao ya kielimu.

Uongozi wa Shule ya Sekondari Mwatulole umeeleza kuwa msaada huo utasaidia kuharakisha ukamilishaji wa uzio wa shule na kuboresha zaidi mazingira ya usalama kwa wanafunzi na jamii inayozunguka shule hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!