Latest Posts

WAZIRI BASHUNGWA AAGIZA JESHI LA POLISI KUDHIBITI MAANDAMANO NA MATISHIO YA KIUSALAMA NCHINI

Na; mwandishi wetu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Innocent Bashungwa amesema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania litaendelea kuwawezesha wafungwa na mahabusu kusikiliza mashauri yao wakiwa magerezani kupitia ‘Mahakama Mtandao’, hasa kunapokuwepo na viashiria vya matishio ya kiusalama ili kudumisha amani na kulinda usalama wa raia na mali zao

Ameeleza kuwa mojawapo ya sababu ya kuendelea kutumia ‘Mahakama Mtandao’ ni masuala ya kiusalama, ambapo hivi karibuni baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametoa matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani na usalama, hali iliyosababisha baadhi ya wafungwa na mahabusu kusikiliza mashauri yao kwa njia ya mtandao

Bashungwa ameyasema hayo, tarehe 30 Aprili 2025 jijini Dodoma alipoambata na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kukagua makasha ya kisasa ya ‘Mahakama Mtandao’ yanayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya kiteknolojia katika Gereza la Isanga, Dodoma

“Jeshi la Polisi linapokuwa na taarifa za kiinterejensia za wazi na zisizo wazi, kwa mfano maandamano ya CHADEMA, na Watanzania ni mashahidi, viongozi wa CHADEMA walisema waziwazi kwamba wataandamana wakakinukishe, Jeshi linapokuwa na taarifa za kiusalama likashirikiana na Mahakama kutoa haki ile ile lakini kwa kutumia teknologia ya ‘Mahakama Mtandao’ ili kuzuia fujo mtaani, naomba Watanzania watuelewe” -Bashungwa

Aidha, Waziri Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha kuna utulivu kwa kudhibiti maandamano, matishio ya kiusalama, na vitendo vyote vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi

“Niendelee kuliagiza Jeshi la Polisi  kusimamia sheria na kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na amani, hata yule ambaye hataki amani, sisi tutamlazimisha kuhakikisha nchi yetu inakuwa amani na salama” -Bashungwa

Pia, Bashungwa ameliagiza Jeshi la Magereza kusimamia kwa ukamilifu sheria na taratibu kwa wale wanaotaka kuwaona wafungwa na mahabusu akieleza kuwa taratibu hizo lazima ziheshimiwe bila upendeleo

“Niliona moja ya viongozi akisema anataka ‘special treatment’ anapoenda kumuona mahabusu, hiyo nayo sio sawa, zipo taratibu zinazosimamiwa ndugu, jamaa na rafiki anapotaka kwenda kumuona mahabusu au mfungwa, kwahiyo mkitaka tuwe na ‘VIP treatment’ na yenyewe sio sawa” -Bashungwa

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Vita Kawawa amelipongeza ya Jeshi la Magereza kwa kuendelea kuwawezesha wafungwa na mahabusu kupata haki zao kwa kusikiliza mashauri kupitia ‘Mahakama Mtandao’, hatua inayotekeleza mapendekezo ya ‘Tume ya Haki Jinai’.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!