Latest Posts

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AKABIDHIWA OFISI NA UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya Jenista Mhagama Agosti 16, 2024 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Jenista amempongeza Ummy Mwalimu kwa uongozi wake ndani ya Wizara ya afya kwa kipindi chote alichofanya kazi ndani ya Sekta ya Afya kwa miaka 14.

“Nakupongeza Ummy Mwalimu hakika maendeleo haya ya Sekta ya Afya una mchango mkubwa katika kuifikisha Sekta ya Afya hapa ilipo, tutaendelea kushirkiana na kupeana ushauri zaidi katika kazi”, amesema Waziri Mhagama.

Akikabidhi Ofisi Ummy Mwalimu amempongeza Jenista Mhagama kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Afya.

“Umekuwa Kiongozi mwenye uzofu wa kutosha ndani ya Serikali naamini kwa uwezo wako ulionao pamoja na timu hii ya Wizara unaweza kuendelea zaidi katika kuboresha Sekta ya Afya nchini”, amesema Ummy Mwalimu.

Viongozi wengine wageni walioshiriki kwenye shughuli hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Ismail Rutamila ambaye pia ameahidi kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na Viongozi katika kuboresha Sekta ya Afya nchini pamoja na Dkt. Irene Isaka, Mkurugeni Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!