Latest Posts

ZAIDI YA MITUNGI 1,000 YA GESI YAGAWIWA DODOMA KUPUNGUZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

Zaidi ya mitungi 1,000 ya gesi imetolewa jijini Dodoma kwa taasisi za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari, vituo vya afya, zahanati pamoja na mama lishe na baba lishe. Hatua hii inalenga kupunguza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kuwa jitihada hizo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Mavunde amesisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa ustawi wa jamii na mazingira.

Ikumbukwe kuwa mapema mwaka huu, Serikali ilizindua kampeni ya matumizi ya nishati safi, ikilenga matumizi ya nishati hiyo nyumbani na katika taasisi mbalimbali binafsi na za umma.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesisitiza kuwa kila mtu ana wajibu wa kutumia nishati safi ya kupikia. Amesema hatua hiyo itasaidia si tu kupunguza uchafuzi wa mazingira bali pia kutunza uoto wa asili, ambao ni chanzo muhimu cha mvua.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!