Latest Posts

BIDEN ATAKA HATUA SAWIA BAADA YA SHAMBULIO LA IRAN DHIDI YA ISRAEL

Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema hataki kushiriki katika shambulio lolote kwenye maeneo ya nyuklia ya Iran kufuatia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na Iran dhidi ya Israel. Ametaka Israel kuchukua hatua “sawia” dhidi ya Iran.

Biden alitoa kauli hiyo siku ya Jumatano, ikiwa ni siku moja baada ya Iran kurusha zaidi ya makombora 180 ya masafa marefu. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameapa kuwa Iran italipa gharama. Biden alisema hatua za Israel lazima ziwe na uwiano.

Katika hatua nyingine, duru za ndani za G7 zimeeleza kuwa viongozi wa umoja huo wanapanga kuzungumza na Israel na Iran ili kupunguza mvutano na kuepusha vita vya kikanda. Mazungumzo haya yanatarajiwa kujumuisha majadiliano ya haraka na Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!