Latest Posts

WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MIONGOZO 

 

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kuendelea kuwa na umoja na kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata miongozo ili kuimarisha uchumi wa Njombe.

Kuruthum ameeleza hayo jana March 14 wakati akizungumza na watumishi katika futari ya pamoja aliyoiandaa kwa watumishi waisilamu na wakristu kwa lengo pia la kubadirishana mawazo.

“Ni muda mrefu hatujawahi kuwa pamoja namna hii kwa hiyo tukaona ni busara na jambo jema wote waisilamu na wakristu tukiwa tumefumefunga basi tuweze kushiriki chakula cha jioni kwa pamoja”amesema Kuruthum

Erasto Mpete ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema Tanzania haina dini lakini wananchi wake wana dini hivyo kupitia mkusanyiko huo wameendelea kukumbushana kuwa wamoja.

“Wote tunaamini Mungu kwa hiyo mkusanyiko huu unatukumusha kuwa sote ni wa moja kwa hiyo jukumu letu ni kujenga taifa la Tanzania”amesema Mpete

Baadhi washiriki wa futari hiyo akiwemo Enosy Lupimo pamoja na Ichikael Malisa wameshukuru uongozo wa halmashauri kwa kuwakutanisha na kuahidi kuendelea kuwa wamoja kwa maslahi ya halmashauri na wananchi wa Njombe.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!