Latest Posts

SERIKALI ITUMIE UWEZO WA SEKTA BINAFSI KUPATIKANA OKSIJENI YA TIBA

Serikali imeombwa kuzipa nafasi kampuni binafsi zenye uwezo wa kuzalisha oksijeni ya tiba kwa ajili ya hospitali, badala ya kuwekeza zaidi katika ujenzi wa mitambo mipya ya uzalishaji.

Ombi hilo limetolewa leo Agosti 17, 2026 jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases PLC, Daniel Warungu, akisema kampuni hiyo ina uzoefu na uwezo mkubwa wa kuzalisha oksijeni salama na yenye ubora kwa matumizi ya afya.

Warungu amesema TOL Gases inaendelea kuongeza uwezo wa uzalishaji kupitia miradi mikubwa, ikiwemo kituo kipya cha kutenganisha hewa (ASU) kitakachoanza kufanya kazi Oktoba 2026 na kuongeza uzalishaji wa oksijeni hadi takribani tani 20 kwa siku.

Aidha, amesema mapato ya kampuni yaliongezeka kutoka Sh bilioni 30.2 mwaka 2024 hadi Sh bilioni 31.15 mwaka 2025, huku faida kabla ya kodi ikipanda kutoka Sh bilioni 3.98 hadi Sh bilioni 6.78.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Leonard Kitoka, amesema Tanzania kwa sasa ina uwezo wa kutosha kutoka kwa wazalishaji binafsi kukidhi mahitaji ya oksijeni ya tiba, hivyo rasilimali za umma zinaweza kuelekezwa zaidi katika kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma hiyo.

TOL Gases imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na Serikali, taasisi za afya na wadau wa maendeleo kuhakikisha upatikanaji endelevu wa oksijeni salama na yenye ubora nchini.

Wanahisa pia wamekubaliana kutogawana gawio, badala yake fedha hizo zitumike kuwekeza katika miundombinu ya kampuni ili kuongeza uzalishaji na mapato.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!