Latest Posts

WAGHANA 62 WAUAWA VITA YA URUSI NA UKRAINE: WAZIRI AINGILIA KATI JIJINI MOSCOW

Serikali ya Ghana imetoa wito wa kutaka kukomeshwa mara moja kwa kitendo cha raia wa mataifa ya Afrika kusajiliwa na kushiriki katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine, kufuatia vifo vya raia wake nchini humo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, amethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya raia 62 wa Ghana wameuawa wakiipigania Urusi katika vita hivyo vya Ukraine, huku raia wengine 15 wakiwa bado hawajulikani waliko.

Bwana Ablakwa ameyasema hayo jijini Moscow alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Urusi kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kidiplomasia na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov.

Amebainisha kuwa matumizi ya raia wa Kiafrika katika uwanja wa mapambano ni jambo linalopaswa kusitishwa mara moja ili kulinda maisha ya raia hao na usalama wa mataifa yao.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na maafisa wa Ukraine, zaidi ya raia 272 wa Ghana wamesajiliwa na kujiunga na jeshi la Urusi tangu kuibuka kwa vita hivyo mwaka 2022.

Tathmini za Serikali ya Ukraine zinaonesha kuwa takribani raia 2,000 kutoka nchi 36 tofauti za Afrika wanapigana katika uwanja wa vita kwa niaba ya Urusi.

Hata hivyo, kwa upande wao, maafisa wa Serikali ya Urusi wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo wakisisitiza kuwa hawawasajili raia kutoka mataifa ya Afrika kinyume na sheria za kimataifa au bila ridhaa yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!