Latest Posts

WAMI/RUVU YAWEKA MIKAKATI KUIKABILI EL NINO | MHANDISI MMASSY ATOA ANGALIZO USAFI WA MITO

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imekutanisha Kikosi Kazi cha Mkoa wa Dar es Salaam na wadau wasafisha mito jijini Dar es Salaam kujadili changamoto zinazoathiri usafi wa vyanzo vya maji na kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Nino zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Mhandisi Elibariki Mmassy akizungumza jijini Dar es Salaam, amesema usafi wa mito ni nguzo muhimu katika kulinda vyanzo vya maji, hivyo ushirikiano wa serikali, sekta binafsi na wananchi unahitajika ili kuzuia kuziba kwa njia za maji, mafuriko na uharibifu wa mazingira wakati wa msimu wa mvua.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru, amesisitiza taasisi na wadau wote kutekeleza wajibu wao kwa wakati ili kuhakikisha mifereji na mito inaendelea kuwa safi, hatua itakayosaidia kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.

Naye Katibu wa CHAWAMADA, Athumani Kambi, amesema wadau wa usafi wa mazingira wako tayari kushirikiana na mamlaka husika katika kuimarisha shughuli za usafi wa mito, huku akieleza kuwa elimu kwa jamii ni muhimu ili kuondoa tabia ya kutupa taka kwenye vyanzo vya maji.

Mkandarasi Shani Ngwanda amesema utekelezaji wa kazi za usafishaji wa mito utaendelea kuzingatia viwango vya kitaalamu, huku akibainisha kuwa ushirikiano wa wadau wote utasaidia kuongeza ufanisi wa hatua zinazochukuliwa kuimarisha usalama wa mazingira na miundombinu wakati wa msimu wa mvua za El Nino.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!