Latest Posts

PRST YATAMBUA MCHANGO WA TANESCO KWA UMMA

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetwaa tuzo nne za umahiri katika mawasiliano kwa umma, zikitambua mchango wake katika utoaji wa taarifa, mawasiliano ya kimkakati na ubunifu wa kuwafikishia wananchi habari kwa ufanisi.

Akizungumza Oktoba 8, 2026, baada ya kupokea tuzo hizo katika Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST), Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Irene Gowelle, amesema mafanikio hayo ni chachu ya kuendelea kuboresha mawasiliano na matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kuwahudumia wananchi.

Amesema TANESCO itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati, huku akishukuru PRST, Wizara ya Nishati, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika kwa mchango wao.

Kwa upande wake, Savera Kazaura, aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ameipongeza TANESCO kwa kuboresha utoaji wa taarifa kwa wananchi, hususan wakati wa changamoto za huduma ya umeme, akizitaka taasisi za umma kuwekeza zaidi katika mawasiliano.

Tuzo zilizotolewa kwa TANESCO ni pamoja na Ubora katika Usimamizi wa Mawasiliano wakati wa Migogoro, Kampeni Bora ya Elimu kwa Umma kupitia kampeni ya Nishati Safi ya Pika kwa Umeme, na Idara Bora ya Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma.

Aidha, Irene Gowelle alishinda tuzo ya Mtaalamu Bora wa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Tanzania kwa mwaka 2026.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!