Latest Posts

TRA KUENDELEA KUIMARISHA VILABU VYA KODI MASHULENI: TOSAMAGANGA KUWA KLABU YA MFANO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Klabu ya Kodi ya Shule ya Sekondari Tosamaganga mkoani Iringa tarehe 30 Oktoba 2026.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidi vifaa hivyo Meneja wa TRA mkoa wa Iringa Bi. Mai Gloria Saria amesema ni natarajio ya TRA kuwa vifaa hivyo vitaongeza ufanisi katika shughuli za klabu ya kodi, ufundiahaji na kujifunza shuleni hapo. Pia amepongeza na kutoa shukrani kwa Kamishna Mkuu wa TRA kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivyo.

“Tunamshukuru sana Kamishna wetu Mkuu Bw. Yusuph Juma Mwenda kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa hivi”. Amesesena Bi. Mai Gloria.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma na Mawasiliano wa TRA Bw. Hudson Kamoga amepongeza uongozi wa shule ya Tosamaganga kwa kuendelea kulea klabu ya kodi na kuwataka wanafunzi kuwa mabalozi wa kodi na kuwa wazalendo wa ulipaji kodi wa hiari.

Aidha Mkuu wa shule ya Sekondari ya Tosamaganga Bw. Raurent Manga amesema TRA wamekuwa wadau muhimu sana katika shule hiyo pia mapato yanayokusanywa na TRA yamesaidia kuboresha miundombinu na utoaji wa elimu bora nchini. Kipekee amempongeza Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda na kusema kuwa naye ni zao la Tosamaganga.

“Kipekee nimpongeze Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda kwa kazi nzuri anayofanya na yeye ni zao la Tosamaganga”. Amesema Bw. Manga

Pia Bw. Manga amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa.

TRA imeanzisha vilabu vya kodi mashuleni na vyuoni ili kuwajengea wanafunzi uelewa juu ya masuala ya kodi na kujua umuhimu wa kodi katika maendeleo ya Taifa ili wawe mabalozi wa kodi na wawe wazalendo wa ulipaji kodi wa hiari. Katika jitihada hizo TRA imekabidhi kompyuta 20 za mezani (Desktop Computers) pamoja na mashine moja ya kuchapisha na kudurufu nyaraka (Heavy duty Printer/Photocopier) kwa klabu ya kodi Tosamaganga.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!