Latest Posts

RC MABULA ATEMBELEA OFISI ZA CCM TABORA, AAHIDI USHIRIKIANO KULETA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Angelina Mabula, ametembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa viongozi wa chama hicho na kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Chama katika kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa na viongozi hao leo Novemba 04, 2026, Dkt. Mabula amesema atashirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa CCM kuhakikisha anatekeleza maelekezo aliyoyapokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutatua changamoto za wananchi.

Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Tabora, akiwemo Hamidi Rashid, wamemuomba Mkuu huyo wa Mkoa kuweka uzito katika kutatua kero zinazowakabili wananchi, ikiwemo migogoro ya ardhi, wakieleza kuwa utatuzi wa changamoto hizo utachochea maendeleo na kuboresha maisha yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!