Latest Posts

RC SENDIGA AWEKA WAZI NAMBA YA KUPOKEA KERO ZA WANANCHI

 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Queen Sendiga, amezindua rasmi namba maalumu ya simu inayolenga kuboresha mawasiliano kati ya wananchi na Serikali pamoja na kurahisisha upatikanaji wa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Sendiga amezindua huduma hiyo Novemba 9.2026 mkoani Morogoro, ambapo amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kero za wananchi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati, akisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wananchi.

Amesema wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanapaswa kutumia namba 0800114045 kuwasilisha kero, malalamiko na changamoto mbalimbali ili ziweze kufanyiwa kazi na mamlaka husika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!