Latest Posts

AMSONS KUTOA BILIONI 95 KUJENGA HOSPITALI 11 ZA MAMA NA MTOTO

Kampuni ya Amsons Group imesaini makubaliano na Serikali ya Tanzania ya kutoa msaada wa Dola za Marekani milioni 38 sawa na takribani Shilingi bilioni 95 za Kitanzania, kwa ajili ya kujenga hospitali 11 maalumu za mama na mtoto katika mikoa tisa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Novemba 26, 2026, wakati wa Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Watoto, Vijana na Lishe (RMNCAH+N), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, chini ya uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Amsons Group itagharamia ujenzi wa hospitali zote 11 kama msaada wa moja kwa moja kwa Serikali bila kuisababishia Serikali mzigo wa deni. Hospitali hizo zitajengwa Dar es Salaam, Ruvuma, Zanzibar, Tabora, Singida, Geita, Songwe, Mwanza na Mara.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group, Edha Nahdi, amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma za dharura kwa wajawazito.

Amesema hospitali hizo zinatarajiwa kuhudumia takribani akina mama na watoto milioni moja kila mwaka mara zitakapokamilika na kukabidhiwa kwa mamlaka za afya za umma.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!