Latest Posts

TANZANIA NA MALAYSIA ZAJADILI FURSA ZITOKANAZO NA TEKNOLOJIA

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeungana na taasisi nyingine serikalini ikiwemo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenye kongamano maalum la teknolojia (ICT kwa ujumla wake) lililohusisha mataifa mawili ya Tanzania na Malaysia

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika, Alhamisi Novemba 21.2024, Serena Hotel, jijini Dar es Salaam Daud Liganda ambaye ni Meneja Uhamasishaji uwekezaji wa nje kutoka TIC amesema Malaysia ni miongoni mwa mataifa yanayofanya vizuri kwenye masuala ya teknolojia, na kwa kutambua hilo TIC imeona iko sababu mahsusi ya kuwepo kwa kongamano hilo ikizingatiwa kuwa Duniani kote kwa sasa uwekezaji wa sekta mbalimbali unategemea sana uwepo wa teknolojia/ ICT

Amesema uwepo wa kongamano hilo, unaenda kupanua wigo wa uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili sio tu kwenye sekta ya teknolojia/ ICT bali pia kwenye maeneo mengine ikiwemo Maliasili na utalii, kilimo, biashara nk

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mulembwa Mnaku amesema uwepo wa kongamano hilo kwa kiasi kikubwa unatokana na ukweli kwamba serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu inayo dhamira ya dhati ya kuhakikisha inatoa nafasi ya ukuaji wa uchumi shirikishi unaokwenda sambamba na masuala ya ubunifu, teknolojia/ ICT na masuala mengine yanayoshabihiana na hayo.

Ameendelea kufafanua kuwa, anaamini kukamilika kwa kongamano hilo ambalo pia linakutanisha wafanyabishara na wawekezaji wa masuala ya teknolojia/ ICT kutoka hayo mawili ni sehemu ya fursa ya kubadilisha mawazo, ujuzi nk ambao kwa namna moja au nyingine utasaidia kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta husika

Novatus Aggrey ni miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo kutoka kampuni ya Kitanzania ya Neurotech Africa Company Ltd, anasema ushiriki wake hapo anaamini utamsaidia sio tu kuelewa wawekezaji na wafanyabishara wa Malaysia wamefanya nini hadi kufikia hatua waliyopo sasa kwenye sekta ya teknolojia/ ICT bali pia kwake itamsaidia kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza kubadilishana mawazo na ujuzi kwenye nyanja mbalimbali zinazohusu masuala hayo

Naye, mmoja wa washiriki wa kongamano hilo kutoka nchini Malaysia amesema anaamini uchumi wa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla wake umekuwa ukikua kwa kasi kwa miaka ya hivi karibuni hivyo ni nafasi ya pande zote mbili sasa kujadili na kufikia muafaka ili kwa pamoja waweze kuona njia gani sahihi wanayoweza kutumia ili kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zitokanazo na teknolojia, ICT.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!